Cheka kidogo

ANGALIA MZUNGUKO WA SAA YAKO.

Kuna mtu mmoja alifariki dunia na akaenda kwa Mungu,alipofika akakuta saa za ukutani nyingi sana zimetundikwa. Akauliza 'Hivi hizi saa ni za nini huku?' Akajibiwa na Askofu mkuu aliyemkuta huko, 'Kila saa ina dhambi za kila Binadamu,ikizunguka mara moja ina maana ametenda dhambi mara moja'.

Yule jamaa akauliza 'mbona hii hapa imesimama ni mbovu? Akaambiwa hiyo ni ya mama Theresa, na inamaanisha kuwa hakutenda dhambi kabisa ndio maana imesimama.

Jamaa ikabidi aulize tena, 'hivi saa ya Edward Lowasa na Ballali iko wapi kati ya hizi?' akajibiwa, 'ya hao ndugu iko ofisini kwa Bwana Yesu mwenyewe maana anaitumia kama feni kwa jinsi inavyozunguka mara nyingi na kwa kasi.'

0 Response to "Cheka kidogo"

Powered by Blogger