KaRuMe, MkApA, kIkWeTe

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kulia),Rais Karume(kushoto) na Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa wakibadilishan mawazo baada ya kumalizika Hitma ya Mama yake Dk shein,iliyofanyika jana katika msikiti wa Kwaboko Mjini Zanzibar.

BaDo NiPo

Leo nimemsikiliza Mwana FA na kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la Bado nipo nipo,kwa kweli kazi hii inaongea ukweli na ukweli bado nipo nipo,tembelea www.bongo5.com ama http://www.bongo5.com/content/view/4401/203/lang,en/.

Chabo


Brain!


siku Alikiba alipokamua London.......


picha kwa hisani ya mdau wetu wa london...jane

Miaka 10 Ya Fm Acadeia

wadau waifurahia kinywaji cha heineken
kwasi machine kama kawaida
askofu alan akionyesha ufundi wake


mdau wenu nae alikwepo


hapa def defao na wanenguaji wake



hakuna aliyebaki kwenye kiti




hatimaye pengo la vijisenti lazibwa!


pichani dk.kawamba,aliyeteuliwa kushika wadhifa aliokuwa nao mzee wa vijisenti..chenge.

Cheka kidogo

GAY TERRORIST


CHEKA KIDOGO!

A Saudi being interviewed at the US Embassy.

Consul: "Your name please?"
Saudi: "Abdul-Aziz."
Consul: "Sex?"
Saudi: "Six times a week."
Consul: "I mean, male or female?"
Saudi: "Both male and female sometimes even camels."
Consul: "Holy cow!"
Saudi: "Yes, cows & dogs too."
Consul: "Man, isn't that hostile?"
Saudi: "Horse style, dog style, any style!"
Consul: "Oh dear!"
Saudi: "Deer? No deer, they run too fast...!"

THE KENYA POLICE


KAMANDE PETER KINYANJUI

PAYSLIP


MONTH: JUNE 2007


Basic Salary 15,000

Hse allowance 0

Gross salary 15, 0000


Deductions


Magereza SACCO 3000.00


NHIF 320.00


NSSF 200.00


PAYE 2740.00


Loan repayment 3260.00


KCB LOAN 2250.00


Total Deductions 11770.00


Net Pay 3230.00

BREAKING NEWZZZZZZZ......

BILIONEA CHENGE AJIUZULU

KWAHERI DITTO

Pichani ni Mwili aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri ukipakiwa katika gari tayari kupelekwa katika chumba cha kuifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro mchana huu mara baada ya kufariki dunia ghafla kwenye Hotel ya Hilux mjini Morogoro.Kifo chake kimethibitishwa na mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa, Dk. Meshack Mmasi ambaye amesema alimpokea marehemu akiwa ameshafariki.

bongo tambarale

MWANANYAMALA IONEKANAVYO LEO ASUBUHI BAADA YA MVUA ZA JANA USIKU.





najua mnajua ila hii ni muhimu kujua zaidi

HABARI ZA KUTHIBITIKA!

Ufisadi WA Samwel Sitta

Ama kweli, ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni!
Kama unadhani vigogo wa EPA ni mafisadi peke yao ,
basi ulikuwa hujamfahamu Spika wa Bunge SAMUEL JOHN
TEGEZA SITTA ! Ukimsikiliza anapoongea unaweza kuamini
kwamba kiongozi huyo wa Bunge ni msafi kutokana na
umahiri wake wa kujivalisha sifa kemkem – Mr Misifa.

Unakumbuka hivi karibuni alivyomtukana Naibu Spika eti
hawezi kusimamia mambo nyeti mpaka awepo yeye mwenye
Bunge? ! Kisa nini? Kupenda sifa na kumdhalilisha
mwenzake mbele ya umma, halafu bado anaendelea kuliita
Bunge eti ni chombo cha kidemokrasia!

Tumebaini kwamba Sitta amekuwa akijimiminia sifa
nyingi ili kulinda ufisadi anaoufanya usigundulike
katika jamii yetu. Ngoja nikupe tone tu la madhambi
yake kwa umma ili uone ni hatua gani utachukua, na ili
na yeye ajipime kwa nafasi yake. Angalia uchafu huu:--


Anatumia vibaya fedha za umma. Amekuwa akitumia
msaidizi wake kuchota mapesa kwa kisingizio kuwa ni
masurufu ya safari za ndani na nje ya nchi. Kila
safari ya siku moja ndani ya nchi huchukua shilingi
Milioni tano (5,000,000/=), na kila safari ya siku
moja nje ya nchi huchukua shilingi Milioni Kumi na
Tano
(15,000,0000/=).

Ameshindwa kufanya marejesho ya masurufu (imprest)
hayo, licha ya kupeleka risiti kadhaa za kughushi/za
uongo kwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge. Mpaka sasa
anadaiwa jumla ya shilingi Milioni sitini
(60,000,000/=) za masurufu.-

SITTA hupeleka risiti za uongo kwa Mhasibu Mkuu,
zikionesha madai kutoka Oysterbay Pharmacy ya Shilingi
Milioni Mbili (2,000,000/=) aliyotumia kwa tiba kila
wiki.- Amekuwa akilazimisha hawara yake wa Hospitali
ya Aga Khan naye alipwe posho kama wabunge anapokwenda
naye Dodoma. Kwa mfano, hawara huyo alilipwa 'per
diem' kuanzia tarehe 13/12/2007 hadi tarehe 31/01/2008
(Siku 50). Huo ni Ufisadi mkubwa!

Anaye kimada wake mwingine anayekwenda kwa jina la
ASIA ambaye anaishi nyumba Na. 111 karibu na
Mahakama ya Ardhi Upanga na amezaa naye. Huko mtaani
kwao kimada huyo hujiita mama SITTA, na ni dada yake
aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa iliyokuwa Tume ya
Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC). Mwanamke huyo
muda wote hutumia gari la Ofisi ya Bunge STK 232
Toyota RAV 4.

Pia anaye kimada mwingine (jina limehifadhiwa) ambaye
anaishi kinondoni (Livingstone), mtaa wa Honolulu
katika nyumba ya kupanga nayomilikiwa na dada yake
Kawawa. Nyumba hiyo inatazamana na Nyumba Na.
KH.MK/No. 337 katika mtaa huo huo. Kimada huyo hutumia
gari ya kiofisi ya Spika mwenyewe STK 3002.- Vimada
wote hao hupata huduma za maji na umeme kwa gharama za
Ofisi ya Bunge.

Kuna kipindi mke halali wa Spika, aliwahi kulalamikia
hali hiyo. Kuna siku maji yalikatika nyumbani, mke wa
Spika akaomba apelekewe ' bowser' la maji na Ofisi ya
Bunge. Ohooo! Watekelezaji wakapeleka maji kimakosa
kwa kimada. Mama Sitta akashtukia dili.

Kuna taarifa kwamba mnamo Mwezi Oktoba 2007, Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali PAC) iligundua mapungufu
makubwa katika matumizi ya fedha yaliyofanywa na Spika
SITTA. nimedokezwa kuwa Spika aliwanyamazisha wajumbe
wa kamati hiyo, ambapo aliwatishia kutowapatia posho
na safari za nje kama wangeyafumua mapungufu yake
hadharani! Hapo inaonesha kuwa wajumbe hao walipewa
rushwa!!

Kama JK anataka viongozi wa kisiasa na wa serikali
watenganishe biashara na uongozi wa ku – 'sacrifice'
kimojawapo, hilo litakuwa gumu kwa sababu Sitta
alipokuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha cha
Uwekezaji nchini (TIC) alitumia nafasi hiyo kuingia
ubia na wafanyabiashara wengi wa Kigeni. Je, Wizara
ya Maliasili na Utalii inatambua kuwa Spika ana hisa
kwenye kampuni moja ya Kichina inayosafirisha nagogo
licha ya marufuku yaliyowekwa?!

Nililokupa hapo ni tone tu.

chenge atua bongo kujibu mapigo

Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge akijibu mwasali ya waandishi wa habari juu ya shutma za kujilimbikizia fedha muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana mchana akitokea nchini China katika alikokuwa ziarani na Rais jakaya Kikwete

BBC Kusaka wafanyabiashara vijana


BBC inatafuta vijana wenye mawazo ya kibiashara kushiriki katika shindano lijulikanalo kama Faidika na BBC, litakalozinduliwa rasmi Jumatatu Aprili 21 2008.

Faidika na BBC inaalika vijana wanaozungumza Kiswahili, na wenye umri wa kati ya miaka 16 hadi 24, kuwasilisha michanganuo yao, ya jinsi ya kuanzisha biashara ambayo itanufaisha jamii. Mchanganuo huo utatakiwa kuwiana na bajeti ya Dola za Marekani 5,000, zitakazotolewa, ikiwa ni zawadi ya kwanza na kuwa msingi wa biashara hiyo. Mchanganuo usizidi maneno 1,500. Michanganuo itumwe kwa: faidika na BBC, PPF Building, 8th Floor, P.O Box 79545, Dar es Salaam. Au kwa barua pepe: faidika@bbc.co.uk.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Solomon Mugera, amesema "Shindano hili ni fursa kwa vijana wenye kuona mbali, na ni nafasi yao ya kutimiza ndoto zao. Hii pia ni nafasi kwa vijana kujisaidia wao wenyewe na jamii zao kwa ujumla".

Salim Kikeke, Meneja Mradi wa Faidika na BBC ameongeza "Nina imani kuwa vijana wengi wana mawazo mazuri na ya kuvutia ya kibiashara. Kwa wale ambao hawatashinda zawadi ya kwanza, tutajitahidi kuwatafutia ushauri wa kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao".

Kutakuwa na mchuano wa kutafuta mshindi mmoja kutoka kila nchi. Kuna jumla ya nchi sita zinazoshiriki katika shindano hili. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Mchuano wa kutafuta mshindi wa Rwanda na DRC utafanyika kwa siku moja. Mchuano wa Tanzania utafanyika Jumatano tarehe 4 mwezi Juni. Mshindi kutoka nchi husika atazawadiwa cheti maalum na kombe.

Washindi sita, mmoja kutoka kila nchi zilizoshiriki, watapambana kuwania nafasi ya kwanza mjini Kampala, Uganda, Jumatano, tarehe 18 Juni. Fainali hiyo itatangazwa moja kwa moja kupitia matangazo ya jioni ya BBC, Dira ya Dunia, na vilevile katika mtandao kupitia bbcswahili.com. Mshindi atapata dola elfu tano za Marekani, pamoja na Kombe. Jopo la majaji litaundwa na wafanyabiashara vijana kutoka Afrika Mashariki na Kati.

David Ssegawa, kijana mwenye umri wa miaka 22, raia wa Uganda, alikuwa mshindi wa Faidika na BBC mwaka jana baada ya kuwashinda washiriki wengine zaidi ya 5,000, kutoka eneo la Afrika Mashariki na kati, wanaozungumza Kiswahili. David aliandika mchanganuo wa utengenezaji mishumaa. Hivi sasa amekwisha anza biashara yake na inaendelea vizuri. Kupata habari zaidi kuhusu David Ssegawa, pamoja na shidano la Faidika na BBC ingia katika mtandao wetu bbcswahili.com.
Powered by Blogger