mambo yetu yaleee

Kuna hiki kiumbe dhaifu lakini cha ajabu hapa duniani
>kiitwacho mwanaume. Ni cha ajabu kutokana na uwezo
>wake wa kubadilika kufuatana na mazingira kilichomo
>kwa wakati husika. Hakika hata yule bingwa wa
>kujibadili kinyonga haoni ndani. Angalia kwa mfano
>mazungumzo ya simu ya kiumbe hiki.
>
>Miaka kama kumi nyuma wakati kikifahamika kwa sifa ya
>'mchumba wa mtu':
>"Sweetheart! Habari za asubuhi"
>"Nzuri tu dear, sijui wewe !"
>"Aa, mimi hali yangu sio nzuri kabisa"
>"Ee nini tena Dear !"
>"Nimekumiss mpenzi wangu, halafu usiku mzima wa jana
>nakuota tu!"
>"Jamani pole sana mpenzi"
>"Asante lakini haitoshi darling ! Hivi kwanza leo
>nitakuona saa ngapi?"
>"Sijui wewe labda unifuate wakati wa lanchi !"
>"Ok basi, wife to
be endelea na kazi huku ukiendelea
>kukumbuka ule wimbo wangu ninaoupenda kukuimbia !"
>"Mh? Upi tena huo dear ?"
>"Aaah unaniangusha darling ! Si ule wa oh my sweet,
>my sugar, let melove you forever, oo yes!, umeukumbuka
>?!"
>"Alaa! Huo! Basi nimeukumbuka! Bye dear!"
>"Bye, nibusu basi"
>"Baadaye dear, kuna watu hapa!"
>"Ok basi!"
>
>Haya basi miaka kumi na mbili na watoto wanne baadaye
>hiki kiumbe mwanaume sasa kina hadhi ya 'mume wa mtu'
>na sasa tunakutana nacho kikipiga simu kwa yulee mtu
>aliyekuwa mchumba wake miaka kumi na mbili nyuma na
>ambaye sasa anakwenda kwa hadhi ya "mkewe". Mazungumzo
>yaokwenye simu sasa ni "makavu" kama mtumba wa Manzese
>........!
>
>"Hujambo ?"
>"Sijambo ! Za kazi ?"
>"Safi, hawajambo hao ?"
>"Hawajambo tu !"
>"Huyu aliyekuwa anaharisha vipi ?"
>"Anaendelea vizuri, nimempa
enthoromycin naona
>inamsaidia"
>"Sawa huyo fundi wa TV naye kishafika ?"
>"Sijamuona !"
>"Sawa, akija muangalie sana asiibe vitu kwenye hiyo
>TV !"
>"Sawa, sasa Baba nanii...!"
>"Unasemaje?"
>"Kuhusu ile losheni"
>"Umeshaanza! Nimesema nitakununulia!"
>"Jamani Baba nanii.....! Mwezi wa pili huu sasa, kila
>siku unaniambia hivyo hivyo!"
>"Alaa! Tumeshaanza kuhesabiana siku sasa!"
>"Basi yaishe ! Mimi nilikuwa nakukumbusha"
>"Haya, mimi nitachelewa kurudi nyumbani kidogo kuna
>jamaa naenda kumcheki nikitoka kazini !"
>"Sawa"
>"Baadaye basi"
>"Sawa"
>Kiumbe kiitwacho mwanaume kinamaliza kuongea na mkewe
>na kukata simu.Bila shaka utapata taabu kukubali
>kwamba huyo ndiye yule yule aliyekuwa anaongea kwenye
>simu ya kwanza miaka kumi na mbili iliyopita. Bila
>shaka pia utajiuliza, yako wapi manenoyale
'darling',
>sweetheart', mpenzi na wimbo wa 'ooh my sweet my
>sugar!' sasa yamekuwa ni bidhaa adimu mdomoni mwa mume
>na masikioni kwa mkewe. Lakini ni kweli kwamba maneno
>hayoyamekuwa bidhaa adimu kwenye mdomo wa kiumbe hiki,
>mume ?
>
>Hebu tusikilize simu hii ya mwisho ya kiumbe huyu
>dakika chache tu baada ya kuongea na mkewe anaongea na
>simu hii akiwa amevua ile hadhi ya mume na kujivika
>mwenyewe bila kushurutishwa na mtu, hadhi ya buzi na
>anayeongea naye ni kiumbe mwenye hadhi ya mchuna buzi.
>Patamu hapo, babu yangu!
>
>"Haloo, darling!"
>"haloo mambo"
>"Poa! Unafanya nini sasa hivi darling wangu?!"
>"Aaa nipo tu natengeneza nywele zangu!"
>"Yees ! Zitengeneze vizuri ule mtindo ninoupenda,
>jioni nitapita hapo nikupeleke ukapate vikuku na
>vikopo viwili vitatu!"
>"Sawa darling ! Halafu dear, vipi kuhusu vile
vitenge
>vya Zaire wanavyopitisha wale kinamama niliokuambia!?"
>"Darling na wewe ! Si nilishakwambia wakipitisha tena
>we chukua tu pea mbili halafu uniambie tu mimi
>nitakupa pesa?!"
>"Asante ! Na vile viatu je ?"
>"Darling sasa unataka kuniudhi ! Nimeshakuambia kuwa
>sio lazima uniombe ruksa kila kitu ! We chukua halafu
>unaniambia mi nakupa hela, sawa ?"
>"Sawa mpenzi, nashukuru! Sasaaaa?"
>"Wee endelea kujitayarisha, mi nikimaliza tu kazi
>hapa nakuja kukupitia, au vipi !"
>"Sawa halafu nakumiss ile mbaya!"
>"Mi pia"
>"Asuu, haayo maumbile yako yananipendeza!"
>"Jamani mpenzi ! Hivi wenzako hawakusikilizi kweli
>hapo!?"
>"Watajaza ! Asuu roho ingekuwa nguo ningekuazima
>univae hadi mileleeeeee....!"
>"Bwana hebu acha!"
>"Ok basi darling, tutaonana baadaye!"
>"Haya, dear!"
>Mpsyuuuuuuuuuuuuuu!"
>"Asante
darling!"
>"Asante darling!"
>
>
> Naona tuishie hapa kwanza maana tayari kuna baadhi ya
>wanaume wameshaanza kuuchuna na kununa, kwa vile simu
>hizi tatu "zimewagusa"kiaina. Kazi kwao. Ujumbe wetu
>uko pale pale; wanaume, wake zenu wanastahili pia hizo
>'darling', 'oh my sweet', 'honey', mpenzi,
>'sweetheart' na 'asuu kila kilicho cha kwangu wewe
>chukua', mnazowapa wasiostahili ! Mungu kibariki
>kiumbe kinachoitwa mwanaume !.
>
>MWENYE MASIKIO,....................

0 Response to "mambo yetu yaleee"

Powered by Blogger