Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara yazuru kampuni ya tcc
Bw.Paul Makanza (kulia) akifafanua jambo kwa Mbunge wa Rombo Mh Basil Mramba.
Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC, Bw.Paul Makanza ( kulia) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,mara baada ya kutembezwa kiwandani humo na kujionea mashine za kisasa kabisa zinavyofanya kazi na kuzalisha bidhaa za kampuni hiyo.
Menejea uzalishaji wa kampuni ya Sigara TCC,Bw.David Nderimo akielezea namna bidhaa zao zinavyotengenezwa kiwandani hapo mbele ya Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara.Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC ,Bw.Paul Makanza (kulia) akiuongoza ujumbe maalumu wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara uliozuru kiwandani hapo mapema leo asubuhi.
Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni ya TCC,Bw.Simon Matta akifafanua jambo mbele ya ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,anaefuata ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Mh.Mbarouk Mwandoro pamoja na Mh Basil Mramba ambaye pia ni Mbunge wa Rombo wakisikiliza kwa makini.
Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC ,Bw.Paul Makanza akifafanua jambo mbele ya Uongozi wa kampuni hiyo pamoja na ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara mapema leo asubuhi ndani ya ofisi za kampuni hiyo .
Mapema leo asubuhi kampuni ya Sigara TCC ilitembelewa na ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,kwa madhumu ya kutathmini ufanisi/utendaji wa kazi na maendeleo kwa ujumla ya Kampuni hiyo.Pichani kama uonavyo ni baadhi ya Uongozi wa kampuni hiyo pamoja na kamati husika wakijadiliana mambo mbalimbali ndani ya ofisi za kampuni hiyo zilizopo barabara ya Nyerere,jijini Dar.
0 Response to "Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara yazuru kampuni ya tcc"
Post a Comment