WAKALA WA M-PESA AUAWA NA MAJAMBAZI!



Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika


WAKAZI watatu wa jijini Dar-es-Salaam akiwemo mwanafunzi wa wa chuo kikuu cha Dar-es-Salaam wanashikiliwa na polisi,Mkoani Singida kwa tuhuma za kumpiga Wakala wa M-pesa risasi wa mjini Singida,Bwana Stephen Rwemamu (37) na kusababishia kifo chake papo hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,Kamanda wa polisi Mkoani Singida,Bi Celina Kaluba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja naTuruka Abert @ Philipo (27),mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati,Sebastian Colman (17) mwanafunzi wa sekondari ya Gosteli mkazi wa Mwenge na John Josephati @ Mangili (32) mkazi wa Mwenge mfanyabiashara na mwanafunzi wa chuo kikuu ambaye anachukua masomo ya uhandisi.

Kwa mujibu wa kamanda hauyo watuhumiwa hao wanatuhumiwa kumuua mfanyabiashara Rwemamu ambaye pia alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya simu (TTCL) Mkoani hapa,kwa kumpiga risasi moja kifuani,juni sita mwaka huu saa 3.45 usiku,kwenye maeneo ya mtaa wa Minga,katika Manispaa ya Singida.

Aidha msemaji huyo wa jeshi alisema mke wa marehemu aliyetambulika kwa jina la Rehema Maswa alitoa taarifa juu ya kuuawa kwa mume wake na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi mara tu baada ya kuteremshwa na teksi aliyokuwa ameikodi kurudishwa nyumbani.

Hata hivyo Kaluba aliweka bayana kwamba wauaji hao wametumia silaha aina ya bastola.

Alifafanua pia kamanda Kaluba kuwa baada ya taarifa hizo kutolewa polisi,ndipo SSP Wankyo akiwa anaongozana na askari wengine,leo asubuhi (jana) walipekua nyumba ya kulala wageni ya Mbacho chumba cha Califonia na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watatu.

Kamanda huyo hata hivyo alibainisha kuwa katika upekuzi huo, walifanikiwa kukamata bastola moja yenye namba CZ-83 aina ya broningm AO 64356 na risasi zake 47.

Alisema hadi sasa chanzo cha mauaji hayo, bado hakijafahamika na watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wo wote upelelezi utakapokamilika.

0 Response to "WAKALA WA M-PESA AUAWA NA MAJAMBAZI!"

Powered by Blogger