NI Aibu"

The Land of Kilimanjaro, Olduvai, Serengeti, Tanganyika, Zanzibar, Ufisadi and Uchawi!.... of course there are exceptions!
Na ndiyo ukweli wenyewe kwa baadhi ya WaTz.
Wametusema sawasawa.

Nchi ya wachawi?

Na ndiyo maana bado tunabishana kuhusu nani ameficha kiatu cha kukimbilia, wakati wenzetu wameshajipanga kwenye mstari. Na tukishakipata kiatu cha pili tunacholitafuta, kiatu cha kwanza watakuwa wajinga fulani fulani wanaojiona werevu sana wamekificha ama wamekitoboa. Yaani ali munradi tuna visingizio gunia tele.
Kazi tumekalia kusema na kuamini uchawi, uvivu, kusemana, kutafutana visa, kuomba omba na kuamini miujiza tuuuuuu badala ya kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa. Yaani mtu anaamini kabisa kuwa atapataga mautajiri ya fasta fasta kwa ulozi. Hata anayejitahidi kufanya kazi anaogopa kutishwa kulogwa. Yaani ni aibu mfanowe hakuna.

Dawa?
Elimu inayoendana na wakati na mazingira. We mtu anafundishwa nadharia tu shuleni, vipindi vya vitendo, maabara hamna vifaa ya kutosha ama hakuna kabisa vifaa, anaishia kukariri tu, sasa huyu mtu akihitimu atatarajiwa vipi afanye kazi kwa ufanisi? Ndiyo usanii tena unakuja bila kutaka. Maneno meeengi, kuagiza kwiiingi, lakini mwambie akuonyeshe kwa mfano kwa vitendo..... utasikia, 'fanya tuu', 'yaani hujui', 'hiyo rahisi', Ningejua ningeuliza? Shule ndiyo zimeshakuwa sehemu za kukulia tu sasa na kujifunza ujamaa! Maanake walimu wanasema utajifunza utapoanza kazi!


Wengine wenu mtanichukia tu lakini ndiyo hivyo tena, nimeshayasema mawazo yangu, kwani nimekulazimisha ukubali? Hatufanani!

0 Response to "NI Aibu""

Powered by Blogger