Uingereza yazidisha masharti kwa wageni

UINGEREZA imeongeza masharti ya kupatikanaji wa viza zake na kuweka adhabu ya kifungo cha miaka 10 ya kutoingia nchini humo kwa waombaji wa viza watakaobainika kughushi nyaraka.

Afisa Habari wa Ubalozi wa Uingereza nchini, John Bradshaw jana alisema kuwa, alisema adhabu hiyo itakayotolewa duniani kote, itaanza kutumika kuanzia Aprili mosi mwaka huu.

" Aprili mosi mwaka huu, mtu yeyote ambaye huko nyuma aliwahi kuvunja sheria zetu za uhamiaji na kwenda nchini Uingereza kinyume cha sheria au kutumia udanganyifu katika maombi ya viza atapigwa marufuku kuingia Uingereza kwa kipindi cha kufikia hadi miaka kumi," alisema Bradshaw.

Bradshaw alitaja mambo yanayoweza kumsababishia mtu adhabu hiyo kuwa ni kufanya kazi nchini Uingereza kinyume cha sheria, kuishi siku 28 zaidi ya muda ulioonyeshwa kwenye viza yake, kwenda nchini humo kinyume cha sheria na kughushi nyaraka katika kutuma maombi ya viza.

Alisema nchi hiyo imeamua kutoa adhabu hiyo ili kudhibiti ongezeko la vitendo vya kutumia nyaraka za kughushi kwa waombaji wa viza wanaotaka kwenda Uingereza wanaotumia nyaraka za kughushi nchini.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2006/2007 pekee asilimia 17 ya watu 562,556 walioomba viza za Uingereza walinyimwa kutokana sababu mbalimbali ikiwamo kughushi vyeti ambapo nchini Tanzania asilimia ya watu walionyimwa vyeti hivyo ni 16.

Katika hatua nyingine, Ubalozi huo nchini umeanzisha mfumo mpya wa uandaaji na upatikanaji wa viza ambapo kuanzia sasa viza zitapatikana siku ya kazi inayofuata badala ya siku moja kama ilivyo awali.

Bradshaw alisema hilo limesababishwa na uongezeko la uhitaji wa kufanya uchunguzi zaidi kiusalama ambapo sasa uchunguzi huo unafanyika kutoka sehemu moja (Centralised), Uingereza

0 Response to "Uingereza yazidisha masharti kwa wageni"

Powered by Blogger