ccj wamvaa waziri marmo!!!!
Na Mwandishi wetu.
CHAMA Cha Jamii CCJ kimemshukia Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Uratibu na Bunge) Philip Marmo, kwa kutumia ofisi yake vibaya kwa kuingilia ofisi ya Msajili pamoja na Chama na kumuita ni sawa na mpiga debe vituo vya basi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu Bara, Dickson Ng’hily katika makao makuu ya chama hicho Mwananyamala jijini Dar es Salaam,kufuatia taarifa zilizoripotiwa katika vyombo vya habari juu ya CCJ kutopatiwa usajili wa kudumu kwa kuchelewa kufanya hivyo.
Nghily alisema kwa kauli alizotoa Waziri Marmo ni za kichochezi kwa Watanzania wapendamaendeleo hasa katika dhama hizi za ukweli na uwazi.
“Kauli aliyoitoa kwa kiongozi kama yeye ni ya kipuuzi na isiyo na mantiki kwa watanzania, yeye hana mamlaka ya kumsemea msajili wa vyama, kufanya hivyo ni sawa na mpiga debe na mvurugaji wa ukweli” alisema Nghily.
Aliendelea kusema kuwa, kwa taarifa alizonukuliwa waziri huyo ikiwemo ya Tendwa anaonewa, alidai kuwa yeye ndiye anayemuonea Tendwa kwa kuingilia mamlaka yasiyo muhusu.
“Marmo ndiye anayemuonea Tendwa kwa kumuingilia ofisi yake, Ofisi ya Msajili hipo huru iweje Waziri kama yeye aingilie chombo hicho huru?” alihoji na kutolea mfano kuwa, Marmo anamfunika Tendwa pastiki alafu anamwambia apite katika moto pasipokujua madhara atakayoyapata; alimalizia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Richard Kiyabo, alisema kuwa wanashangazwa na kauli hizo alizotoa Waziri Marmo na kuziita kuwa ni za kichonganishi kwani tena bila kufanya uchunguzi.
“Kama anasema ofisi ya Msajili haina fedha ya kufanya uhakiki wa usajili na fedha zilisha pitishwa na Bunge, hilo yeye aliliongea kisiasa na anatakiwa aombe radhi kwa kuingilia uhuru wa chombo hicho cha usajili” alisema Kiyabo.
Mbali na Kiyabo, kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Renatus Mwabhi, aliwataka wanachama wa CCJ kuipuuza kauli hiyo kwani haina manufaa na zaidi imejaa Siasa.
“Sisi tuaongoza kisayansi, na si kama hao viongozi wanaokulupuka kila siku na kutoa kauli za utatanishi’ alisema Mwabhi.
Aidha, Mwabhi alisema kuwa CCJ mpaka sasa kimejiimalisha na kinauhakika wa kupata usajili huo wa kudumu kuanzia sasa, baada ya Ofisi ya Msajili kuwapa taratibu za uhakiki wa wanachama kwenye mikoa mine , huku kwa Dar es Salaam uhakiki unatarajia kuanza kesho Juni 3, katika viwanja vya Mwembe Yanga.
CCJ ilidai kuwa, ilikuwa katika hatua za mwisho kuipa notisi ya siku ofisi ya Msajili kama ingeshindwa kuendelea taratibu za usajili.
‘Tulikuwa na kusudio la kuipa notisi ya siku saba, ambayo tulikuwa tunaipeleka ambapo ilikuwa na lengo la kumfungulua kesi na kusimamishwa mambo yote ya Uchaguzi, lakini alituita na kutuomba radhi kwa kuchelewa” alisema Mwabhi.
Katika kauli yake hiyo, Mwabhi alisema Tendwa aliamua kuwaomba radhi CCJ kwa kusema kuwa, “Tendwa alihudhunika kufuatia kupokea ujumbe wa simu zaidi ya 300, ukimtaka ahalakishe usajili ambapo alisema ulimfedhehesha sana” alinukuu kauli ya Tendwa.
Kufuatia ofisi ya msajili kuanza mikakati ya uhakiki na kuanza na mikoa mine, ambapo mikoa hiyo ni Dar es Salaam Juni 3,Pwani Juni 4, Morogoro Juni 5 huku kwa upande wa Zanzibar uhakiki huo unatarajia kufanyika Juni 9 Unguja Magharibi.
“Tunaomba wanachama wote wa CCJ kujitokeza kwa wingi katika mikoa hiyo ilituweze kuhakikiwa na kuharakisha harakati za kupata usajili wa kudumu, tunahakika zoezi ili litafanyika mapema na kupata usajili wetu”.
Pia aliwaomba CCJ kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mwembe Yanga ilikufanikisha zoezi hilo la Uhakiki.
“Tunataka kumuonyesha Tendwa kuwa CCJ si chama cha kuchezea, afike afanye uhakiki na kisha kusonga katika mikoa hiyo iliyobaki hadi na kisha kutupa mikoa mingine ya Tanzania nzima” alisema.
0 Response to "ccj wamvaa waziri marmo!!!!"
Post a Comment