Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh.Parseko Kone akifungua Sherehe ya Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.John Chiligati ambaye pia ni mbunge wa Singida Jimbo la Manyoni(wa pili kulia) katika Hoteli ya Regency Park jijini Dar es Salaam,Kutoka kushoni ni Mh.Martha Mlata Mbunge Viti maalum Singida,Mwenyekiti wa Makampuni ya Mohammed Enterprise Bw.Ghulam Dewji baba mzazi wa Mbunge wa Singida Mjini,Mh.Mohammed Dewji katika Sherehe hiyo.
Mh.John Chiligati akikabidhi Pesa Taslimu Shilingi Milioni moja zilizochangwa na Wabunge wote wa Mkoa wa Singida kwa ajili ya Kuwapongeza Vijana wa Kindai Shooting Stars baada ya kutwaa Ubunge wa Kili Taifa Cup 2010 kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh.Parseko Kone katika Hotel ya Regency Park jijini Dar es Salaam wakati wa Chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Mh.John Chiligati anayeshuhudia tukio hilo Kulia ni Mbunge wa Singida Kaskazini Mh.Misanga.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh.Parseko Kone akipokea Fedha Taslimu Shilingi Milioni 5 ikiwa ni ahadi iliyotolewa Mh.Mohammed Dewji endapo watashinda Kutwaa Ubingwa wa Kili Taifa Cup 2010 anaye kabidhio fedha hizo ni Baba Mzazi wa Mbunge wa Singida Mjini Bw.Ghulam Dewji aliyemwakilisha mwanaye katika Hafla hiyo.(katikati)Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.John Chiligati.
Mbunge wa Singida Viti Maalum Mh.Martha Mlata akiongea na Vijana wa Kindai Shooting Stars(hawapo pichani) kuwapa moyo vijana hao baada ya kuitangaza Vyema mkoa wa Singida kwa kunyakua Ubingwa wa Kili Taifa Cup 2010 ikiwa ni kama Historia tokea Mwaka 1974 walikuwa wakifikia hatua za fainali bila ubingwa lakini kwa mwaka huu 2010 Singida imevunja rekodi kwa kutwaa Ubingwa huo.Mh.Mlata alitoa Shilingi laki 5 kama changamoto kwa Vijana hao waweze kuendelea Vizuri na Mshindano yajayo.
Mdau wa Soka Nchini Bw.Samwel Nakei (Mkandarasi) ambaye ni mzaliwa wa Singida aliguswa sana na Ushindi huo na yeye pia aliwapatia Vijana wa Kindai Shooting Stars Fedha Taslimu shilingi milioni 5 kama Changamoto kwa Vijana wa Mkoa aliotokea yeye.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Parseko Kone akimkabidhi Kaptain wa Timu ya Singida Kindai Shooting Stars Idrisa Rashi bahasha ya Pesa ambazo ni zawadi kutoka Wabunge wa Mkoa huo pamoja na wadau mbalimbali wa Soka Nchini.
Kocha wa Timu ya Kindai Shooting Stars Bw.Suleiman Matola akiwaongoza Vijana wake wa Timu ya Kindai Shooting Stars kupata Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mh.John Chiligati kuwapongeza Vijana hao baada ya kuwaletea Ushindi Mkoa wao katika Hotel ya Regency Park jijini Dar es Salaam jana.
Vijana wakindai Shooting Stars wakipata dinner la Usiku lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Vijana baada ya Kutwaa Ubingwa wa Kili Taifa Cup 2010.
Viungo wa timu ya Kindai Shooting Stars wakipiga msosi wa Nguvu jana katika Hotel ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Mkoa wa Singida na wadau mbalimbali kattika picha ya Pamoja na Timu ya Singida Kindai Shooting Stars inayotokea Jimboni kwa Mh.Mohammed Dewji.
Bw.Kassim Dewji Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Mkoa wa chama cha mpira Singida akiteta jambo na Mh.Chiligati pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa Chakula cha jioni jana katika Hotel ya Regency Park.Kutoka kushoto ni Mbunge wa Singida Viti Maalum Mh.Martha Mlata naye akiteta jambo na baba mzazi wa Mh.Mohammed Dewji Bw.Ghulam Dewji.
0 Response to "Mh.Mohammed Dewji atimiza ahadi yake kwa Timu ya Kindai Shooting Stars!"
Post a Comment