wajumbe kamati kuu wapiga kura



Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume wakitoka nje wa ukumbi wa mkutano wa Kizota wakati wa mapumziko mafupi ili kutoa nafasi ya kura kuhesabiwa.

Kitenge Na Hando Ndani Ya South Kuiona Brazili Na Ureno



Watangazaji mahiri Maulid Kitenge wa Radio One Stereo na Gerald Hando wa Clouds FM kesho watapata bahati ya kushudia pambano kali la soka katika fainali za Kombe la Dunia kati ya Brazil na Ureno.

Balozi Kupela azungumzia miaka 35 ya uhuru wa msumbiji!!!



Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Amour Zacarias Kupela (kulia) leo jijini Dar es salaam ameongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya kusherehekea miaka 35 ya Uhuru wa Msumbijiambayo itaadhimishwa kesho (june 25, 2010.) Mwengine ni Afisa wa Ubalozi wa Msumbiji nchini (1 st Secretary )Rashide Ussuale. Pamoja na kuzungumzia siku ya maadhimisho ya Uhuru wa MSUMBIJI, Balozi Kupela amezungumzia masuala ya mafanikio ya miradi mabalimbali zikiwemo nyanja za kuinua uchumi. miundombinu,kilimo,madini, utalii,huduma za afya,elimu pamoja na vita vya kupambana kuondoa umaskini .

Maisha club kufunguliwa wiki hii



Askari wa zimamoto wakipambana na moto ulioteketeza Maisha Club maeneo ya Oysterbay jijini Dar mnamo Novemba 8, 2009. Habari za uhakika ambazo Globu ya Jamii inazo zinasema kwamba baada ya ukarabati mkubwa Maisha Club inatarajiwa kufunguliwa upya wiki hii na kuleta sura ingine katika viota vya maraha jijini Dar. Mmiliki wa Maisha Club, Mama Hellen Sweya, kesho anakutana na wanahabari kutangaza tarehe ya uzinduzi wa club hiyo

RAIA WA OMAN ABAMBWA NA MADAWA YA KULEVYA TABORA!

Jeshi la Polisi mkoani Tabora, linawashikilia watu wawili akiwemo Raia mmoja wa Oman kwa tuhuma za kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Heroin.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Kamishna Msaidizi Liberatus Barlow, amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Mbaraka Hemedi(34) Raia wa Oman na Mohammed Sharifu(41) Mtanzania mwenye asili ya Kiarabu.

Amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa huko Wilayani Igunga mkoani Tabora baada ya Raia wema kuwatonya Polisi juu ya kuwepo kwa watuhumiwa hao kwenye gari aina ya Toyota Chesser lenye namba za usajili T. 676 ANM huku wakijigunga sindano zenye madawa hayo.Amesema baada ya Polisi kuwakamata walifanya upekuzi zaidi ndani ya gari hilo na kufanikiwa kupata kete 18 za madawa hayo aina ya heroin ambayo thamani yake bado kufahamika mara moja.

Hata hivyo, Kamanda Barlow amesema tayari Makachero wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi mkoani humo ACP David Ambwene Mwakiruma, wamejikita zaidi katika utafuta wa taarifa za muhimu ili kubaini chimbuko la mtandao mzima unaojihusisha na biashara hiyo ya madawa ya kulevya.

“Lakini tunafanya Uchunguzi zaidi kuweza kuwa na uhakika wa chanzo cha madawa haya kwa sababu kwa mkoa wetu ni mara ya kwanza kufanikisha kukamatwa kwa madawa haya ya aina ya Heroin”. Amesema Kamanda Barlow.
Kamanda Barlow ameongeza kwamba kukamatwa kwa madawa hayo kunaonyesha wazi kuwa mikoa ya katikati mwa nchi nayo kwa hivi sasa haiko salama na huwezi ukaitofautisha na maeneo ya mikoa mingine kama ya Pwani na maeneo yanayopakana na nchi jirani.

Amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Polisi na Raia na kwamba watuhumiwa hao wasingeweza kukamatwa kama sio taarifa za uhakika zilizotolewa kwa wakati muafaka ma raia wema wanaojitolea kupiga vita vitendo vya kihalifu hapa nchini.Kamanda Barlow amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya.

rais kikwete ana kwa ana na Bill Clinton ikulu leo



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na katika mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton Ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.

sherehe za miaka 10 ya twanga pepeta juni 27, 2010




Mkurugenzi wa ASET Da' Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye mgahawa wa Hadees wakati alipozungumzia maandalizi ya sherehe za miaka kumi ya bendi yake ya African Stars inayotarajiwa kufanyika Juni 27 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa msanii wa n ngoma za asili kutoka Kenya anayeitwa Tonni Nyandudo.

Asha amesema kutafanyika maadamano yatakayowahusisha wanamuziki wa bendi hiyo pamoja na marafiki wa bendi hiyo maadamano yatakayoanzia katika ofisi za ASET na kuishia katika viwanja vya Leaders na kufuatiwa na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu, kukimbiza kuku, kuruka kamba , kuvuta kamba na kukimbia na magunia.

Baada ya michezo hiyo kutafuatia na onyesho kubwa litakalofanywa na bendi ya Africa Stars itakayopiga nyimbo zake kumi zilizobeba Albam zake hizo kumi huku wanamuziki kadhaa walioanzisha bendi ama kuwahi kufanya kazi katika bendi hiyo hiyo wakishiriki katika onesho hilo.

Amezitaja nyimbo zitakazopigwa na Albam zake kuanzi albam ya kwanza kuwa ni Kisa cha Mpema, Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari 2005 Passworld, Mtaa wa kwanza na Mwana Dar es salaam huku kiingilio katika onesho hilo kikiwa ni shilingi 5000 kwa wote.

Wanamuziki waliokuwa wanzilishi wa bendi ya African Stars walikuwa ni Abuu Semuhando, Jesca Charles, Lwiza Mbutu, Bob Gad, Amigolas, Yahya Mkango, Jose Watuguru, Rogat Hega, Victor Mkambi, Adorf Mbinga na Banza Stone ambaye amethibitisha kushiriki katika onesho hilo.

Wengine waliopo katika picha kutoka kulia ni Abuu Semuhando Katibu wa Bendi na Lwiza Butu ambaye ni kiongozi wa bendi.

VUVUZELA MPYA


mwanaidi hassan ndiye mwanamichezo bora 2009



Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu akimkabidhi tuzo na zawadi ya sh. milioni moja, mwanamichezo Bora wa TASWA, Mcheza Netiboli wa timu ya Taifa na JKT Mbweni, Mwanaid Hassan katika hafla iliyofanyika punde kwenye Hoteli ya New Afrika, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshindi wa tatu, mnyenyua vitu vizito, David Nyombo na Golikipa wa Simba, Juma Kaseaja. Anmayeshuhudia ni Mwenyekiti wa TASWA, Boniface Wambura

JK Ziarani Rukwa



JK akikagua zao la mahindi yanayouzwa katika soko la kimataifa la mazao wilayani Mpanda, mkoa wa Rukwa jana.Pembeni ya Rais ni ofisa wa kilimo Bwana Fredrick Mlowe

RAIS KIKWETE ZIARANI KIGOMA,AZINDUA LAKE TANGANYIKA HOTEL!!!



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma leo mchana

Mkutano Arusha



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akifungua Mkutano wa siku 5 kuhusu,miradi ya Jamii kwa nchi zinazoendelea,katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha leo,mkutano huo umewashirikisha wajumbe wa nchi 45 Dniani.

Ghana Imejiandaa Kuishangaza Dunia Ya Kandanda!



Jioni hii Ghana wanajitupa uwanjani kupambana na Serbia. Kwa muda mrefu imefikiriwa kuwa Ivory Coast ni timu ambayo ingeweza kufanya vema zaidi wakati fainali za Kombe la Dunia zikifanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza. Lakini kwa sasa hali si hiyo. Ghana inaonekana imejiandaa vema kuwashangaza wengi kwa kufika mbali zaidi ya jirani zao Ivory Coast.
Powered by Blogger