WASANII MNAKARIBISHWA KUJA KUSHOOT KWENYE PUB YANGU.


Ben Kinyaiya anawakaribisha wasanii wote na watu wengine kutembelea Pub yake iliyopo nyuma ya Mango Garden Kinondoni. Kwa wale wasanii wanaopenda ma graffiti sehemu hii utachakugua mpaka uchoke.

Kama hili utakutananalo kwa nje limetulia tuliiiiiiiii....

Kuna kaunta ya nje na ya ndani, hii ni kaunta ya ndani ikiwa inamaliziwa maliziwa. Huku VIP unakula kipupwe safiiiiiii huku ukicheki tv yako iliyounganishwa na Dstv.

WANANCHI 300 WAVAMIA KITUO CHA POLISI HEDARU NA KUCHOMA MOTO!


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema akizungumza na waandishi wa habari mchana huu kwenye makao makuu ya jeshi hilo wakati alipozungumzia uvamizi wa kituo cha polisi cha Hedaru uliofanywa na wananchi 300 baada ya kuvamia kituo cha polisi na kuchoma moto pamoja na magari matatu na nyaraka mbalimbali kituoni hapo.

Akifafanua zaidi IGP Said Mwema amesema mnamo tarehe 28-5-2010 mtoto mdogo aitwaye Garce Garce Kelvin mwenye umri wa miaka 5alitoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha akiwa anatokea shule ya chekechea katika mji mdogo wa Hedaru, baadae katika hatua za ufuatiliaji zilipokelewa taarifa kuwa mtot huyo amepelekwa katika kijiji cha Chome Mlimani katika msitu wa Shengena ambako pia kuna machimbo ya Dhahabu kwa imani za kwamba huenda ameenda kutolewa kafara huko kwa imani za kishirikina.

Tarehe 30-5-2010 mkuu wa kituo akiongozana na wapelelezi walifuatilia taarifa hizo zilizopokelewa kutoka kwa wananchi ambapo katika oparesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wapatao sita na waliendelea kuhojiwa katika kituo cha polisi Same.

Mnamo tarehe 31-5-2010 kulitokea kundi lingine la vijana waliokwenda katika msitu wa Shengena kijiji cha Chome ikidaiwa walipata taarifa kwamba mtoto huyo amepelekwa kutolewa kafara kwenye machimbo ya dhahabu kwa imani za kishirikina, hata hivyo vijana hawa hawakufanikiwa kumpata mtoto badala yake waliwakamata watu nane wanaume saba na mwanamke mmoja waliowakuta na vifaa vya uchimbaji wa madiniya dhahabu na kuwapeleka kituo cha polisi Hedaru.


Majira ya saa mbili usiku tarehe hiyohiyo watuhumiwa wakiw akituoni Hedaru uvumi ulizagaa kwamba watu waliokamatwa na kundi la vijana ndiyo waliohusika na kutoweka kwa Grace Kaelvin hivyo kundi la wananchi 300 walivamia ktuo cha polisi na kuchoma moto kwa nia ya kutaka kuwauwa watuhumiwa hao, hata hivyo hakuna vifo vilivyotokea baada ya polisi kufanikisha kuwatorosha watu hao , leo tarehe 162010 mtoto Grace aliyetoweka aliokotwa sokoni eneo la Pasua na kwasasa anapelekwa kuungana na familia yake zaidi yahapo watuhumiwa watano wamekamatwa kwa kuchoma kituo.

Mwema amesema tabia ya kushambulia vituo vya polisi kwa hisia au kuchukua sheria mkononi kunavuruga amani na utulivu nchini, lakini pia ni uvunjaji wa sheria

Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara yazuru kampuni ya tcc


Bw.Paul Makanza (kulia) akifafanua jambo kwa Mbunge wa Rombo Mh Basil Mramba.
Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC, Bw.Paul Makanza ( kulia) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,mara baada ya kutembezwa kiwandani humo na kujionea mashine za kisasa kabisa zinavyofanya kazi na kuzalisha bidhaa za kampuni hiyo.
Menejea uzalishaji wa kampuni ya Sigara TCC,Bw.David Nderimo akielezea namna bidhaa zao zinavyotengenezwa kiwandani hapo mbele ya Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara.Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC ,Bw.Paul Makanza (kulia) akiuongoza ujumbe maalumu wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara uliozuru kiwandani hapo mapema leo asubuhi.
Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni ya TCC,Bw.Simon Matta akifafanua jambo mbele ya ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,anaefuata ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Mh.Mbarouk Mwandoro pamoja na Mh Basil Mramba ambaye pia ni Mbunge wa Rombo wakisikiliza kwa makini.
Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC ,Bw.Paul Makanza akifafanua jambo mbele ya Uongozi wa kampuni hiyo pamoja na ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara mapema leo asubuhi ndani ya ofisi za kampuni hiyo .
Mapema leo asubuhi kampuni ya Sigara TCC ilitembelewa na ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,kwa madhumu ya kutathmini ufanisi/utendaji wa kazi na maendeleo kwa ujumla ya Kampuni hiyo.Pichani kama uonavyo ni baadhi ya Uongozi wa kampuni hiyo pamoja na kamati husika wakijadiliana mambo mbalimbali ndani ya ofisi za kampuni hiyo zilizopo barabara ya Nyerere,jijini Dar.

uzinduzi wa one by one leo

Cheni Arts creation leo 28/5 ndani ya ukumbi wa grm production watzindua movie yao, ONE BY ONE Kuanzia mishale ya jioni.

CARNIVAL 2010

cheka kidogo

KaRuMe, MkApA, kIkWeTe

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kulia),Rais Karume(kushoto) na Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa wakibadilishan mawazo baada ya kumalizika Hitma ya Mama yake Dk shein,iliyofanyika jana katika msikiti wa Kwaboko Mjini Zanzibar.

BaDo NiPo

Leo nimemsikiliza Mwana FA na kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la Bado nipo nipo,kwa kweli kazi hii inaongea ukweli na ukweli bado nipo nipo,tembelea www.bongo5.com ama http://www.bongo5.com/content/view/4401/203/lang,en/.

Chabo


Brain!


siku Alikiba alipokamua London.......


picha kwa hisani ya mdau wetu wa london...jane

Miaka 10 Ya Fm Acadeia

wadau waifurahia kinywaji cha heineken
kwasi machine kama kawaida
askofu alan akionyesha ufundi wake


mdau wenu nae alikwepo


hapa def defao na wanenguaji wake



hakuna aliyebaki kwenye kiti




hatimaye pengo la vijisenti lazibwa!


pichani dk.kawamba,aliyeteuliwa kushika wadhifa aliokuwa nao mzee wa vijisenti..chenge.
Powered by Blogger