Kitenge Na Hando Ndani Ya South Kuiona Brazili Na Ureno
Watangazaji mahiri Maulid Kitenge wa Radio One Stereo na Gerald Hando wa Clouds FM kesho watapata bahati ya kushudia pambano kali la soka katika fainali za Kombe la Dunia kati ya Brazil na Ureno.
Balozi Kupela azungumzia miaka 35 ya uhuru wa msumbiji!!!
Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Amour Zacarias Kupela (kulia) leo jijini Dar es salaam ameongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya kusherehekea miaka 35 ya Uhuru wa Msumbijiambayo itaadhimishwa kesho (june 25, 2010.) Mwengine ni Afisa wa Ubalozi wa Msumbiji nchini (1 st Secretary )Rashide Ussuale. Pamoja na kuzungumzia siku ya maadhimisho ya Uhuru wa MSUMBIJI, Balozi Kupela amezungumzia masuala ya mafanikio ya miradi mabalimbali zikiwemo nyanja za kuinua uchumi. miundombinu,kilimo,madini, utalii,huduma za afya,elimu pamoja na vita vya kupambana kuondoa umaskini .
Maisha club kufunguliwa wiki hii
Askari wa zimamoto wakipambana na moto ulioteketeza Maisha Club maeneo ya Oysterbay jijini Dar mnamo Novemba 8, 2009. Habari za uhakika ambazo Globu ya Jamii inazo zinasema kwamba baada ya ukarabati mkubwa Maisha Club inatarajiwa kufunguliwa upya wiki hii na kuleta sura ingine katika viota vya maraha jijini Dar. Mmiliki wa Maisha Club, Mama Hellen Sweya, kesho anakutana na wanahabari kutangaza tarehe ya uzinduzi wa club hiyo
RAIA WA OMAN ABAMBWA NA MADAWA YA KULEVYA TABORA!
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Kamishna Msaidizi Liberatus Barlow, amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Mbaraka Hemedi(34) Raia wa Oman na Mohammed Sharifu(41) Mtanzania mwenye asili ya Kiarabu.
Amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa huko Wilayani Igunga mkoani Tabora baada ya Raia wema kuwatonya Polisi juu ya kuwepo kwa watuhumiwa hao kwenye gari aina ya Toyota Chesser lenye namba za usajili T. 676 ANM huku wakijigunga sindano zenye madawa hayo.Amesema baada ya Polisi kuwakamata walifanya upekuzi zaidi ndani ya gari hilo na kufanikiwa kupata kete 18 za madawa hayo aina ya heroin ambayo thamani yake bado kufahamika mara moja.
Hata hivyo, Kamanda Barlow amesema tayari Makachero wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi mkoani humo ACP David Ambwene Mwakiruma, wamejikita zaidi katika utafuta wa taarifa za muhimu ili kubaini chimbuko la mtandao mzima unaojihusisha na biashara hiyo ya madawa ya kulevya.
“Lakini tunafanya Uchunguzi zaidi kuweza kuwa na uhakika wa chanzo cha madawa haya kwa sababu kwa mkoa wetu ni mara ya kwanza kufanikisha kukamatwa kwa madawa haya ya aina ya Heroin”. Amesema Kamanda Barlow.
Kamanda Barlow ameongeza kwamba kukamatwa kwa madawa hayo kunaonyesha wazi kuwa mikoa ya katikati mwa nchi nayo kwa hivi sasa haiko salama na huwezi ukaitofautisha na maeneo ya mikoa mingine kama ya Pwani na maeneo yanayopakana na nchi jirani.
Amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Polisi na Raia na kwamba watuhumiwa hao wasingeweza kukamatwa kama sio taarifa za uhakika zilizotolewa kwa wakati muafaka ma raia wema wanaojitolea kupiga vita vitendo vya kihalifu hapa nchini.Kamanda Barlow amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya.
rais kikwete ana kwa ana na Bill Clinton ikulu leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na katika mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton Ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.
sherehe za miaka 10 ya twanga pepeta juni 27, 2010
Mkurugenzi wa ASET Da' Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye mgahawa wa Hadees wakati alipozungumzia maandalizi ya sherehe za miaka kumi ya bendi yake ya African Stars inayotarajiwa kufanyika Juni 27 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa msanii wa n ngoma za asili kutoka Kenya anayeitwa Tonni Nyandudo.
Asha amesema kutafanyika maadamano yatakayowahusisha wanamuziki wa bendi hiyo pamoja na marafiki wa bendi hiyo maadamano yatakayoanzia katika ofisi za ASET na kuishia katika viwanja vya Leaders na kufuatiwa na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu, kukimbiza kuku, kuruka kamba , kuvuta kamba na kukimbia na magunia.
Baada ya michezo hiyo kutafuatia na onyesho kubwa litakalofanywa na bendi ya Africa Stars itakayopiga nyimbo zake kumi zilizobeba Albam zake hizo kumi huku wanamuziki kadhaa walioanzisha bendi ama kuwahi kufanya kazi katika bendi hiyo hiyo wakishiriki katika onesho hilo.
Amezitaja nyimbo zitakazopigwa na Albam zake kuanzi albam ya kwanza kuwa ni Kisa cha Mpema, Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari 2005 Passworld, Mtaa wa kwanza na Mwana Dar es salaam huku kiingilio katika onesho hilo kikiwa ni shilingi 5000 kwa wote.
Wanamuziki waliokuwa wanzilishi wa bendi ya African Stars walikuwa ni Abuu Semuhando, Jesca Charles, Lwiza Mbutu, Bob Gad, Amigolas, Yahya Mkango, Jose Watuguru, Rogat Hega, Victor Mkambi, Adorf Mbinga na Banza Stone ambaye amethibitisha kushiriki katika onesho hilo.
Wengine waliopo katika picha kutoka kulia ni Abuu Semuhando Katibu wa Bendi na Lwiza Butu ambaye ni kiongozi wa bendi.
mwanaidi hassan ndiye mwanamichezo bora 2009
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu akimkabidhi tuzo na zawadi ya sh. milioni moja, mwanamichezo Bora wa TASWA, Mcheza Netiboli wa timu ya Taifa na JKT Mbweni, Mwanaid Hassan katika hafla iliyofanyika punde kwenye Hoteli ya New Afrika, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshindi wa tatu, mnyenyua vitu vizito, David Nyombo na Golikipa wa Simba, Juma Kaseaja. Anmayeshuhudia ni Mwenyekiti wa TASWA, Boniface Wambura
JK Ziarani Rukwa
JK akikagua zao la mahindi yanayouzwa katika soko la kimataifa la mazao wilayani Mpanda, mkoa wa Rukwa jana.Pembeni ya Rais ni ofisa wa kilimo Bwana Fredrick Mlowe
RAIS KIKWETE ZIARANI KIGOMA,AZINDUA LAKE TANGANYIKA HOTEL!!!
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma leo mchana
Mkutano Arusha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akifungua Mkutano wa siku 5 kuhusu,miradi ya Jamii kwa nchi zinazoendelea,katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha leo,mkutano huo umewashirikisha wajumbe wa nchi 45 Dniani.
Ghana Imejiandaa Kuishangaza Dunia Ya Kandanda!
Jioni hii Ghana wanajitupa uwanjani kupambana na Serbia. Kwa muda mrefu imefikiriwa kuwa Ivory Coast ni timu ambayo ingeweza kufanya vema zaidi wakati fainali za Kombe la Dunia zikifanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza. Lakini kwa sasa hali si hiyo. Ghana inaonekana imejiandaa vema kuwashangaza wengi kwa kufika mbali zaidi ya jirani zao Ivory Coast.
KICK-OFF CELEBRATION CONCERT FOR THE 2010 FIFA WORLD AT ORLANDO STADIUM!!!
Patrick Vieira, France’s former national team captain during the 1998 World Cup, (C), World Cup 2010 Local Organizing Comitee Chief excutive officer Danny Jordaan (L) and FIFA Secretary General Jerome Valcke (R) hold the FIFA World Cup trophy at the end of the official Kick off celebration concert on June 10, 2010 at the Orlando stadium in Soweto, Johannesburg.
Colombian singer Shakira performs on stage during the official Kick-off celebration concert of the 2010 FIFA World Cup on June 10, 2010 at the Orlando stadium in Soweto, Johannesburg prior to the start of the football World Cup.
Hitilafu ya magari ya JK wananchi wataka ,Idara za usalama,Ewura kuwajibishwa…!!!
Raisi alikuwa afungue jengo hili jipya la KCB-MOSHI.Mpaka mida ya saa mbili kulikuwa hamna kitu kinachoendelea
miss pwani 2010 waendelea kujifua tayari kwa shindano lao june 12
Mmoja wa washirkji wa shindano la kumtafuta Vodacom Miss Pwani 2010 Shaymaa Edward Mtetema akipozi kwa picha wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika Hoteli ya Raj Kijitonyama , Dar es Salaam jana.
AJALI YA NDEGE....
Ndege aina ya Beaver yenye namba ya usajili 5YBCK inayomilikiwa na shirika la DLCO ikiwa katika mashamba ya miwa kijiji cha Kigenge Turiani wilayani Mvomero Morogoro baada ya kutua ghafla kutokana na kupatwa na hitilafu wakati ikifanya kazi ya kunyunyuzia dawa kwa ajili ya ndege waharibifu (koleakolea) hivi karibuni. Watu wanne walinusurika kifo.
WAKALA WA M-PESA AUAWA NA MAJAMBAZI!
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika
WAKAZI watatu wa jijini Dar-es-Salaam akiwemo mwanafunzi wa wa chuo kikuu cha Dar-es-Salaam wanashikiliwa na polisi,Mkoani Singida kwa tuhuma za kumpiga Wakala wa M-pesa risasi wa mjini Singida,Bwana Stephen Rwemamu (37) na kusababishia kifo chake papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,Kamanda wa polisi Mkoani Singida,Bi Celina Kaluba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja naTuruka Abert @ Philipo (27),mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati,Sebastian Colman (17) mwanafunzi wa sekondari ya Gosteli mkazi wa Mwenge na John Josephati @ Mangili (32) mkazi wa Mwenge mfanyabiashara na mwanafunzi wa chuo kikuu ambaye anachukua masomo ya uhandisi.
Kwa mujibu wa kamanda hauyo watuhumiwa hao wanatuhumiwa kumuua mfanyabiashara Rwemamu ambaye pia alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya simu (TTCL) Mkoani hapa,kwa kumpiga risasi moja kifuani,juni sita mwaka huu saa 3.45 usiku,kwenye maeneo ya mtaa wa Minga,katika Manispaa ya Singida.
Aidha msemaji huyo wa jeshi alisema mke wa marehemu aliyetambulika kwa jina la Rehema Maswa alitoa taarifa juu ya kuuawa kwa mume wake na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi mara tu baada ya kuteremshwa na teksi aliyokuwa ameikodi kurudishwa nyumbani.
Hata hivyo Kaluba aliweka bayana kwamba wauaji hao wametumia silaha aina ya bastola.
Alifafanua pia kamanda Kaluba kuwa baada ya taarifa hizo kutolewa polisi,ndipo SSP Wankyo akiwa anaongozana na askari wengine,leo asubuhi (jana) walipekua nyumba ya kulala wageni ya Mbacho chumba cha Califonia na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watatu.
Kamanda huyo hata hivyo alibainisha kuwa katika upekuzi huo, walifanikiwa kukamata bastola moja yenye namba CZ-83 aina ya broningm AO 64356 na risasi zake 47.
Alisema hadi sasa chanzo cha mauaji hayo, bado hakijafahamika na watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wo wote upelelezi utakapokamilika.
Magari ya Rais yazima tena safarini!!!
Bughudha hizo ziliendelea kuifuata Ikulu jana baada ya tukio hilo kutokea majira ya saa 4:30 asubuhi mjini Moshi na kuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa hapa. Magari hayo yaliweka mafuta kwenye kituo cha Total kinachomilikiwa na mfanyabiashara Epimark Laswai na kusababisha hitilafu hiyo iliyozuia magari hayo kuendelea na msafara.
Magari hayo ya ulinzi yaliyowekewa mafuta kwa ajili ya kujiandaa kwenda Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya kumpokea Rais Jakaya Kikwete, ambaye alitarajiwa kuwasili saa 11:40 jioni.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na maofisa wa vyombo vya dola ziliidokeza Mwananchi kuwa kituo hicho kimewekwa chini ya ulinzi wa polisi na maofisa Usalama wa Taifa na watu watatu wanashikiliwa na polisi.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, mara baada ya magari hayo aina ya Toyota VX V8 rangi nyeusi kuweka mafuta, kifaa maalumu (sensor) ndani ya magari hayo kilibaini kuwa mafuta hayo hayana ubora unaokubalika.
Jitihada za maofisa usalama kuyawasha magari hayo zilishindikana hadi mafundi wa kampuni ya Rajinder Motors walipoitwa na kumwaga mafuta yote yaliyokuwa yamewekwa katika magari hayo.
Habari zaidi zimedai kuwa kituo hicho kimewekwa chini ya uangalizi wa polisi na maofisa usalama hadi wataalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) watakapochunguza ubora wa mafuta hayo.
“Tayari wataalamu wa Ewura wako njiani kuja Moshi kwa ajili ya kuchunguza kituo hicho kama kulikuwa na hujuma kwa msafara wa Rais Kikwete au ni hujuma za uchanganyaji wa mafuta,” kilidokeza chanzo kimoja cha habari.
Mmiliki wa kituo hicho, Epimark Laswai alithibitishia Mwananchi kuhusu tukio hilo na kufafanua kuwa jana asubuhi kituo chake kiliishiwa mafuta na kulazimika kununua mafuta ya dharura kutoka kituo kimoja jijini Arusha.
“Wafanyakazi wangu waliwasiliana na Mount Meru Arusha ambao walituletea lita 4,000 na tulipoyamwaga tu kwenye visima vyetu ndio hayo magari ya Ikulu yakaja yakaweka mafuta na ndio matatizo yote yalipoanzia,” alisema.
Laswai alisema alifanya jitihada kutafuta mafuta mengine masafi ambayo yanaoana na magari hayo na kuhakikisha wafanyakazi wote watatu wa Mount Meru walioshiriki kuleta mafuta hayo, wanawekwa chini ya ulinzi wa polisi.
Mfanyabiashara huyo alisema hata lori lililobeba mafuta hayo limewekwa chini ya ulinzi wa polisi.
Tumeshinda..! NDOVU
Meneja wa Bia ya Ndovu akilonga jambo na wafanyakazi wa TBL na Waandishi wa Habari jioni hii katika viwanja vya TBL muda mfupi mara baada ya kuwasili toka nchini Ujerumani.Pembeni ni Walimbwende waliopamba mapokezi hayo.
Ndovu Special Malt Grand Gold Award Yawasili Nchini
Meneja wa Bia ya Ndovu Oscar Shelukindo (wa nyuma kushoto)na Mpishi Mkuu wa TBL Mzee Gaudence Mkolwe (kulia)wakiwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana wakitokea jijini Wiesbaden nchini Ujerumeni ambako walikabidhiwa tuzo kubwa ya dhahabu ya kinywaji cha Ndovu ijulikanayo kama Grand Gold Award.
TBL Yaadhimisha Siku Ya Mazingira Duniani Leo
Mkuu wa Maswala ya utawala wa TBL,Phocus Lasway (kushoto) akiwa pamoja na Meneja wa Safari Lager,Fimbo Butallah (pili kulia) pamoja na wafanyakazi wengine wa TBL wakishirikiana kufanya usafi leo ikiwa ni siku wa Mazingira Duniani
Mtoto Aliyetekwa.
Mtoto Grace Calvin (5) aliyedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana juzi katika Kata ya Hedaru wilayani Same na kusababisha wananchi kuchoma Kituo cha Polisi na magari matatu
Mourinho sasa ni meneja wa Real Madrid!!
Mourinho atajulishwa kwa mashabiki wa Real siku ya Jumatatu
Klabu kilitoa taarifa kuthibitisha hayo.
Jose Mourinho anaondoka Inter baada ya msimu uliokuwa wa fanaka mno, kupata ushindi katika mashindano matatu muhimu Italia, ikiwa ni pamoja na kuwa klabu bingwa barani Ulaya.
Hata hivyo klabu ya Inter haikutoa maelezo kamili katika taarifa hiyo, kuhusu mapatano hayo kati ya rais wa klabu Massimo Moratti na mwenzake wa Real, Florentino Perez.
KAMATI YA MISS TANZANIA YATEMBELEA MISS DAR CENTRE!!!
Kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi wa Miss Tanzania , chini ya kampuni ya Lino International Agency ambao ndiyo waratibu wa shindano la Miss Tanzania Hashim Lundenga, jana jioni ilitembelea kambi ya Miss Dar City Centre kwenye kambi yao iliyopo katika Hotel ya Lamada.
Kamati hiyo ilikuwa pia na viongozi wengine pamoja na Miss Tanzania Miriam Gerald sasa na mshindi wa pili Beatrice Lukindo wote kwa pamoja waliweza kuwasifia warembo hao na kuwataka wajitahidi kuwakilisha vyema ilikuweza kufikia malengo waliotimiza wao.
Kwa upande wake Lundenga aliwataka warembo hao kujituma na kuacha kusikia maneno ya mitaani juu ya sifa wanazotupiwa mamiss.
“Nawaambieni, mashindano ya Urembo ni sekta ambayo inakuwa kwa kasi mno, hivyo mjitahidi musiitie matope kwa aina yoyote hile, ondoeni dhana zote zilizojengeka”.
Pia aliwasihi mamiss hao kujichunga na kuacha kurubuniwa na wanaume ambao wanataka kuwachezea ambapo hapo baadae wanawaacha.
“Tunaomba ieleweka kuwa, kila mrembo anakuwa chini yetu kuanzia kambi hadi kumalizika kwa kambi, chini ya hapo anakuwa huru, hivyo matukio mabaya juu ya mamis mengi yanawapata wakiwa nje ya utaratibu wetu” alisema Lundenga.
Baadhi ya warembo watakao menyana na kupatikana mshindi wa kituo hicho itakayofanyika katika Hotel ya Movenpick, ni pamoja na Glory Mosha(20), Agness Francice(20),Bahati Chande(20),Kiren Mohammed (20), Sara Nasoro(20),Suraina Merwiro(23), Neena Jackob(2o), Neema Alen(18), Mariam Hassan (19), Sara Said (20),Nance Mane(20) na Anabela Isaya(21).