TGNP na FemAct Yazindua Ilani ya Uchaguzi ya wapiga kura 2010.!!!

Wadau wa (TGNP) na (FemAct) wakiwa kwenye maandamano kuelekea ofisi za (TGNP) kwa ajili ya uzinduzi wa ilani ya uchaguzi wa wapiga kura mwaka 2010 jijini Dar es Salaam.
Proudly sponsored by TIGO.(MIC TANZANIA LTD)

Wadau wa (TGNP) na (FemAct) wakiwa kwenye maandamano kuelekea ofisi za (TGNP) kwa ajili ya uzinduzi wa ilani ya uchaguzi wa wapiga kura mwaka 2010 jijini Dar es Salaam.
Na gazeti la mwananchi.
MJI wa Arusha mwishoni mwa wiki ulizizima baada ya kutokea habari za kifo cha kutatanisha cha mkazi wa Levolosi, Omari Salim, 44, aliyefariki dunia wakati akipelekwa Hosptali ya Mt Meru baada ya kuzidiwa akiwa nyumba ya wageni na mpenzi wake.
Tayari Jeshi la Polisi mjini hapa limeshathibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililoibua maswali mengi kwa wakazi wa mjini hapa. Polisi imedai uchunguzi wa awali umebaini kifo cha marehemu huyo kimetokana na utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu za kiume.
Polisi imezitaja dawa hizo kuwa ni aina ya Muco zilizokutwa ndani ya chumba alichokodi kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Akili Mpwapwa aliiambia Mwananchi kuwa Mei 26 majira ya saa 8;30 Salim alimpigia simu mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Caren Isaack, 20, ili wakutane. Alisema wote kwa pamoja walikubaliana na kwenda kukodi chumba katika nyumba ya kulala wageni ya Rhino.
Alisema baada ya wapenzi hao kuwasili ndani ya chumba hicho, mpenzi wake alimwambia Salim kuwa wapande kitandani kwa lengo la kufanya mapenzi, lakini marehemu alilalamika kuwa alikuwa akijisikia vibaya na ndipo alipoomba kwenda bafuni kuoga.
Kwa mujibu wa Mpwapwa, marehemu aliingia bafuni kuoga, lakini ghafla alitoka akiwa ameshika taulo mkononi huku akitetemeka, ndipo mpenzi wake alipopatwa na mshangao.
Alidai kuwa kadiri muda ulivyokuwa ukienda, ndivyo hali ya Salim ilivyozidi kubadilika na ndipo akaamua kumbeba na kumweka kitandani na baadaye kumfunika shuka, lakini ghafla akaanza kutapika mfululizo.
Kamanda Mpwapwa alifafanua ya kuwa Caren alilazimika kuomba msaada kwa mlinzi wa siku hiyo ndipo walipofanikiwa kumtoa chumbani na kukodi teksi kumuwahisha hospitalini, lakini akakata roho wakiwa wakiwa njiani.
Alidai ya kuwa jeshi la polisi lilikuta vidonge mbalimbali vya dawa zinazosadikiwa kuwa ni za kuongeza nguvu za kiume zilizokuwa katika pakiti na kwamba huenda Salim alimeza vidonge hivyo kabla ya kushiriki ngono.
Kamanda Mpwapwa alisema polisi wanamshikilia Caren kwa uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo


Askari wa usalama barabarani akiangalia mwili wa mkazi wa jiji la Dar es Salaam ambaye hakuweza kufahamika mapema baada ya kugongwa na kichwa cha Treni katika eneo la Daraja la Keko,leo mchana. Imeelezwa kuwa kijana huyo alikuwa akiishi karibu kabisa na eneo hilo ambapo aligeuza eneo hilo kuwa maskani yake ya kudumu, akifanya shughuli zote na kulala chini ya daraja hilo kama nyumbani kwake.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh.Parseko Kone akifungua Sherehe ya Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.John Chiligati ambaye pia ni mbunge wa Singida Jimbo la Manyoni(wa pili kulia) katika Hoteli ya Regency Park jijini Dar es Salaam,Kutoka kushoni ni Mh.Martha Mlata Mbunge Viti maalum Singida,Mwenyekiti wa Makampuni ya Mohammed Enterprise Bw.Ghulam Dewji baba mzazi wa Mbunge wa Singida Mjini,Mh.Mohammed Dewji katika Sherehe hiyo.

Mh.John Chiligati akikabidhi Pesa Taslimu Shilingi Milioni moja zilizochangwa na Wabunge wote wa Mkoa wa Singida kwa ajili ya Kuwapongeza Vijana wa Kindai Shooting Stars baada ya kutwaa Ubunge wa Kili Taifa Cup 2010 kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh.Parseko Kone katika Hotel ya Regency Park jijini Dar es Salaam wakati wa Chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Mh.John Chiligati anayeshuhudia tukio hilo Kulia ni Mbunge wa Singida Kaskazini Mh.Misanga.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh.Parseko Kone akipokea Fedha Taslimu Shilingi Milioni 5 ikiwa ni ahadi iliyotolewa Mh.Mohammed Dewji endapo watashinda Kutwaa Ubingwa wa Kili Taifa Cup 2010 anaye kabidhio fedha hizo ni Baba Mzazi wa Mbunge wa Singida Mjini Bw.Ghulam Dewji aliyemwakilisha mwanaye katika Hafla hiyo.(katikati)Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.John Chiligati.

Mbunge wa Singida Viti Maalum Mh.Martha Mlata akiongea na Vijana wa Kindai Shooting Stars(hawapo pichani) kuwapa moyo vijana hao baada ya kuitangaza Vyema mkoa wa Singida kwa kunyakua Ubingwa wa Kili Taifa Cup 2010 ikiwa ni kama Historia tokea Mwaka 1974 walikuwa wakifikia hatua za fainali bila ubingwa lakini kwa mwaka huu 2010 Singida imevunja rekodi kwa kutwaa Ubingwa huo.Mh.Mlata alitoa Shilingi laki 5 kama changamoto kwa Vijana hao waweze kuendelea Vizuri na Mshindano yajayo.

Mdau wa Soka Nchini Bw.Samwel Nakei (Mkandarasi) ambaye ni mzaliwa wa Singida aliguswa sana na Ushindi huo na yeye pia aliwapatia Vijana wa Kindai Shooting Stars Fedha Taslimu shilingi milioni 5 kama Changamoto kwa Vijana wa Mkoa aliotokea yeye.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Parseko Kone akimkabidhi Kaptain wa Timu ya Singida Kindai Shooting Stars Idrisa Rashi bahasha ya Pesa ambazo ni zawadi kutoka Wabunge wa Mkoa huo pamoja na wadau mbalimbali wa Soka Nchini.

Kocha wa Timu ya Kindai Shooting Stars Bw.Suleiman Matola akiwaongoza Vijana wake wa Timu ya Kindai Shooting Stars kupata Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mh.John Chiligati kuwapongeza Vijana hao baada ya kuwaletea Ushindi Mkoa wao katika Hotel ya Regency Park jijini Dar es Salaam jana.

Vijana wakindai Shooting Stars wakipata dinner la Usiku lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Vijana baada ya Kutwaa Ubingwa wa Kili Taifa Cup 2010.

Viungo wa timu ya Kindai Shooting Stars wakipiga msosi wa Nguvu jana katika Hotel ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Wabunge wa Mkoa wa Singida na wadau mbalimbali kattika picha ya Pamoja na Timu ya Singida Kindai Shooting Stars inayotokea Jimboni kwa Mh.Mohammed Dewji.

Bw.Kassim Dewji Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Mkoa wa chama cha mpira Singida akiteta jambo na Mh.Chiligati pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa Chakula cha jioni jana katika Hotel ya Regency Park.Kutoka kushoto ni Mbunge wa Singida Viti Maalum Mh.Martha Mlata naye akiteta jambo na baba mzazi wa Mh.Mohammed Dewji Bw.Ghulam Dewji.

Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Bara, Dickson Ng’hily wa Chama cha Jamii (CCJ) akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi hizo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam(katikati)Mwenyekiti wa chama hicho Bw.Richard Kiyabo(kulia) Katibu Mkuu wa Chama hicho,Bw.Renatus Mwabhi.
Na Mwandishi wetu.
CHAMA Cha Jamii CCJ kimemshukia Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Uratibu na Bunge) Philip Marmo, kwa kutumia ofisi yake vibaya kwa kuingilia ofisi ya Msajili pamoja na Chama na kumuita ni sawa na mpiga debe vituo vya basi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu Bara, Dickson Ng’hily katika makao makuu ya chama hicho Mwananyamala jijini Dar es Salaam,kufuatia taarifa zilizoripotiwa katika vyombo vya habari juu ya CCJ kutopatiwa usajili wa kudumu kwa kuchelewa kufanya hivyo.
Nghily alisema kwa kauli alizotoa Waziri Marmo ni za kichochezi kwa Watanzania wapendamaendeleo hasa katika dhama hizi za ukweli na uwazi.
“Kauli aliyoitoa kwa kiongozi kama yeye ni ya kipuuzi na isiyo na mantiki kwa watanzania, yeye hana mamlaka ya kumsemea msajili wa vyama, kufanya hivyo ni sawa na mpiga debe na mvurugaji wa ukweli” alisema Nghily.
Aliendelea kusema kuwa, kwa taarifa alizonukuliwa waziri huyo ikiwemo ya Tendwa anaonewa, alidai kuwa yeye ndiye anayemuonea Tendwa kwa kuingilia mamlaka yasiyo muhusu.
“Marmo ndiye anayemuonea Tendwa kwa kumuingilia ofisi yake, Ofisi ya Msajili hipo huru iweje Waziri kama yeye aingilie chombo hicho huru?” alihoji na kutolea mfano kuwa, Marmo anamfunika Tendwa pastiki alafu anamwambia apite katika moto pasipokujua madhara atakayoyapata; alimalizia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Richard Kiyabo, alisema kuwa wanashangazwa na kauli hizo alizotoa Waziri Marmo na kuziita kuwa ni za kichonganishi kwani tena bila kufanya uchunguzi.
“Kama anasema ofisi ya Msajili haina fedha ya kufanya uhakiki wa usajili na fedha zilisha pitishwa na Bunge, hilo yeye aliliongea kisiasa na anatakiwa aombe radhi kwa kuingilia uhuru wa chombo hicho cha usajili” alisema Kiyabo.
Mbali na Kiyabo, kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Renatus Mwabhi, aliwataka wanachama wa CCJ kuipuuza kauli hiyo kwani haina manufaa na zaidi imejaa Siasa.
“Sisi tuaongoza kisayansi, na si kama hao viongozi wanaokulupuka kila siku na kutoa kauli za utatanishi’ alisema Mwabhi.
Aidha, Mwabhi alisema kuwa CCJ mpaka sasa kimejiimalisha na kinauhakika wa kupata usajili huo wa kudumu kuanzia sasa, baada ya Ofisi ya Msajili kuwapa taratibu za uhakiki wa wanachama kwenye mikoa mine , huku kwa Dar es Salaam uhakiki unatarajia kuanza kesho Juni 3, katika viwanja vya Mwembe Yanga.
CCJ ilidai kuwa, ilikuwa katika hatua za mwisho kuipa notisi ya siku ofisi ya Msajili kama ingeshindwa kuendelea taratibu za usajili.
‘Tulikuwa na kusudio la kuipa notisi ya siku saba, ambayo tulikuwa tunaipeleka ambapo ilikuwa na lengo la kumfungulua kesi na kusimamishwa mambo yote ya Uchaguzi, lakini alituita na kutuomba radhi kwa kuchelewa” alisema Mwabhi.
Katika kauli yake hiyo, Mwabhi alisema Tendwa aliamua kuwaomba radhi CCJ kwa kusema kuwa, “Tendwa alihudhunika kufuatia kupokea ujumbe wa simu zaidi ya 300, ukimtaka ahalakishe usajili ambapo alisema ulimfedhehesha sana” alinukuu kauli ya Tendwa.
Kufuatia ofisi ya msajili kuanza mikakati ya uhakiki na kuanza na mikoa mine, ambapo mikoa hiyo ni Dar es Salaam Juni 3,Pwani Juni 4, Morogoro Juni 5 huku kwa upande wa Zanzibar uhakiki huo unatarajia kufanyika Juni 9 Unguja Magharibi.

Mwenyekiti wa chama cha Jamii (CCJ) Bw.Richard Kiyabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya Ofisi hizo.
“Tunaomba wanachama wote wa CCJ kujitokeza kwa wingi katika mikoa hiyo ilituweze kuhakikiwa na kuharakisha harakati za kupata usajili wa kudumu, tunahakika zoezi ili litafanyika mapema na kupata usajili wetu”.
Pia aliwaomba CCJ kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mwembe Yanga ilikufanikisha zoezi hilo la Uhakiki.
“Tunataka kumuonyesha Tendwa kuwa CCJ si chama cha kuchezea, afike afanye uhakiki na kisha kusonga katika mikoa hiyo iliyobaki hadi na kisha kutupa mikoa mingine ya Tanzania nzima” alisema.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema akizungumza na waandishi wa habari mchana huu kwenye makao makuu ya jeshi hilo wakati alipozungumzia uvamizi wa kituo cha polisi cha Hedaru uliofanywa na wananchi 300 baada ya kuvamia kituo cha polisi na kuchoma moto pamoja na magari matatu na nyaraka mbalimbali kituoni hapo.
Na Mwandishi wetu.
MKUU wa jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema ametolea ufafanuzi tukio la wananchi wa Hedaru Wilaya ya Same , Mkoa wa Kilimanjaro, kwa wananchi kuvamia kituo kidogo cha Polisi na kukiteketeza kwa moto pamoja na mali zilizokuwemo kituoni humo,mnamo tarehe 28-5-2010 mtoto mdogo aitwaye Grace Kelvin mwenye umri wa miaka 5 alitoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha akiwa anatokea shule ya chekechea katika mji mdogo wa Hedaru, baadae katika hatua za ufuatiliaji zilipokelewa taarifa kuwa mtoto huyo amepelekwa katika kijiji cha Chome Mlimani katika msitu wa Shengena ambako pia kuna machimbo ya Dhahabu kwa imani za kwamba huenda ameenda kutolewa kafara huko kwa imani za kishirikina.
Tarehe 30-5-2010 mkuu wa kituo akiongozana na wapelelezi walifuatilia taarifa hizo zilizopokelewa kutoka kwa wananchi ambapo katika oparesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wapatao 6 na waliendelea kuhojiwa katika kituo cha polisi Same.
Mnamo tarehe 31-5-2010 kulitokea kundi lingine la vijana waliokwenda katika msitu wa Shengena kijiji cha Chome ikidaiwa walipata taarifa kwamba mtoto huyo amepelekwa kutolewa kafara kwenye machimbo ya dhahabu kwa imani za kishirikina, hata hivyo vijana hawa hawakufanikiwa kumpata mtoto badala yake waliwakamata watu 8 wanaume 7 na mwanamke 1 waliowakuta na vifaa vya uchimbaji wa madiniya dhahabu na kuwapeleka kituo cha polisi Hedaru.
Majira ya saa mbili usiku tarehe hiyo hiyo watuhumiwa wakiwa kituoni Hedaru uvumi ulizagaa kwamba watu waliokamatwa na kundi la vijana ndiyo waliohusika na kutoweka kwa Grace Kelvin hivyo kundi la wananchi 300 walivamia kituo cha polisi na kuchoma moto kwa nia ya kutaka kuwauwa watuhumiwa hao, hata hivyo hakuna vifo vilivyotokea baada ya polisi kufanikisha kuwatorosha watu hao , leo tarehe 1-6-2010 mtoto Grace aliyetoweka aliokotwa sokoni eneo la Pasua na kwasasa anapelekwa kuungana na familia yake zaidi ya hapo watuhumiwa 5 wamekamatwa kwa kuchoma kituo.
Mwema amesema tabia ya kushambulia vituo vya polisi kwa hisia au kuchukua sheria mkononi kunavuruga amani na utulivu nchini, lakini pia ni uvunjaji wa sheria.
Oscar Shelukindo na Mzee Gaudence Mkolwe wakipokea Grand Gold Award ya Ndovu Special Malt jijini Wiesbaden, Ujerumani, usiku kuamkia leo.
Wakiwasili kupoka Grand Gold Award ya Ndovu special malt.
Bw.Paul Makanza (kulia) akifafanua jambo kwa Mbunge wa Rombo Mh Basil Mramba.
Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC, Bw.Paul Makanza ( kulia) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,mara baada ya kutembezwa kiwandani humo na kujionea mashine za kisasa kabisa zinavyofanya kazi na kuzalisha bidhaa za kampuni hiyo.
Menejea uzalishaji wa kampuni ya Sigara TCC,Bw.David Nderimo akielezea namna bidhaa zao zinavyotengenezwa kiwandani hapo mbele ya Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara.
Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC ,Bw.Paul Makanza (kulia) akiuongoza ujumbe maalumu wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara uliozuru kiwandani hapo mapema leo asubuhi.
Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni ya TCC,Bw.Simon Matta akifafanua jambo mbele ya ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,anaefuata ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Mh.Mbarouk Mwandoro pamoja na Mh Basil Mramba ambaye pia ni Mbunge wa Rombo wakisikiliza kwa makini.
Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya TCC ,Bw.Paul Makanza akifafanua jambo mbele ya Uongozi wa kampuni hiyo pamoja na ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara mapema leo asubuhi ndani ya ofisi za kampuni hiyo .
Mapema leo asubuhi kampuni ya Sigara TCC ilitembelewa na ujumbe wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Viwanda na Biashara,kwa madhumu ya kutathmini ufanisi/utendaji wa kazi na maendeleo kwa ujumla ya Kampuni hiyo.Pichani kama uonavyo ni baadhi ya Uongozi wa kampuni hiyo pamoja na kamati husika wakijadiliana mambo mbalimbali ndani ya ofisi za kampuni hiyo zilizopo barabara ya Nyerere,jijini Dar.